0(0)

Uandaaji na Utuzaji wa Taarifa za Kifedha za Biashara Yako

 • Categories BusinessHow to Do
 • Duration 5h 50m
 • Total Enrolled 0
 • Last Update 02/09/2021

Description

Utunzaji kumbukumbu ni mchakato wa kutunza data zinazohusiana na shughuli za biashara
kwenye vitabu vya hesabu. Ni kuandika fedha zote zinazoingia na zinazotoka kwenye biashara
yako.

Kwa wale wenye ndoto za kuwa wafanyabiashara ni vyema wakaanza sasa kukusanya taarifa muhimu za biashara wanazofikiria kufanya. Fuatilia vigezo vyote vinavyohitajika ili kuweza kufanya hiyo biashara. Wakati mwingine inaweza kukulazimu kutafuta ajira katika kampuni inayojihusisha na hiyo biashara unayoiwaza. Pia jiandae kihesabu nikimaanisha kuwa hebu tafuta ujuzi wa kina wa mambo ya mahesabu na jifunze kuandika kila kitu unachofanya na unachopanga kukifanya.

Tambua kuwa mali bila daftari hupotea bila habari. Suala la kuandika kila unachokifanya na unachopanga kukifanya lianze leo hii. Ukimaliza kusoma post hii nenda stationery nunua daftari ama diary. Andika kiasi ulichotumia kununua hiyo diary ama daftari ndani ya hiyo diary ama daftari. Baada ya hapo anza kuandika kila kitu kinachohusiana na mpango wa wewe kujiingiza kwenye biashara.

Andika kuwa umepanga kujifunza kutunza kumbukumbu kwa miezi sita, andika pia kuwa umepanga kujifunza ujasiriamali kwa miezi sita. Andika pia unapanga kujifunza kupitia sehemu gani ama mtu gani. Unaweza amua kuandika ntajifunza ujasiriamali kupitia miamia kwa miezi sita ambapo ntafuatilia na kuwasiliana nao na kuhudhuria semina zao mara kwa mara.

Jiwekee lengo la kutunza kumbukumbu kila mara. Mfano unaweza andika kuwa kuanzia leo matumizi yangu na mapato yangu binafsi ni lazima niyaandike kwenye hii diary ama hili daftari. Tunza salary slip zote. Kila ukinunua tunza risiti zote. Kuna siku ntawaambia umuhimu wa haya makaratasi wakati unatafuta mtaji kwenye mabenki ama wabia wa maendeleo. Pia andika lengo madhubuti la kujifunza. Mfano unaweza andika kuwa ntatafuta maarifa katika tovuti mbalimbali na kutembelea biashara mbalimbali.

What Will I Learn?

 • Kutunza vizuri kumbukumbu na hati za biashara.
 • Kuujua umuhimu na thamani ya kumbukumbu za biashara.
 • Kuzitathmini benki na kuweza kuchagua akaunti ya benki inayofaa.
 • Kuambatisha gharama kwenye bidhaa na kupanga bei na mishahara ambavyo vitawasaidia katika uainishaji.
 • Kujua umuhimu wa orodha ya bidhaa na jinsi ya kuisimamia ili kupunguza gharama.

Topics for this course

11 Lessons5h 50m

Utangulizi

Nini maana ya Taarifa za kifedha za biashara00:15:00
Aina ya taarifa za kifedha za biashara00:10:00

Umuhimu wa uandaaji na utunzaji taarifa za kifedha za biashara yako

Uandaaji wa taarifa za kifedha za biashara

Namna ya utunzaji taarifa za kifedha za biashara

About the instructor

Johnbosco ni mjasiriamali, mtaalamu na mshauri wa kujitegemea wa masuala yahusuyo undeshaji na ukuzaji biashara alie jikita zaidi katika masuala ya kifedha yahusuyo biashara. Pia ni mtaalamu wa masuala ya Mipango biashara, uaandaji na utunzaji wa taarifa za kifedha, na kufanya upembezi yakinifu wa ufanisi katika ukuaji na uendeshaji wa biashara kwa ujumla.
0 (0 ratings)

1 Courses

0 students

Sh 10,000

Material Includes

 • Video za zaidi ya masaa 5 za mafunzo adimu
 • Makabrasha na majedwari ya kuhifadhia mahesabu
 • Pakua Vijitabu vya mafunzo
 • Cheti cha ushiriki

Enrolment validity: 365 days

Requirements

 • Unajua kusoma
 • Unajua kuandika
 • Daftari la mafunzo
 • Graph paper
 • Peni, penseli, ufutio na rula
 • Kikokotozi

Target Audience

 • Wamiliki biashara
 • Benki na asasi nyingine za mikopo
 • Serikali kupitia Wakadiria Kodi
 • Wateja na Umma
 • Waajiriwa au watumishi
 • Washindani

Want to receive push notifications for all major on-site activities?

Jasiri
Logo
Register New Account
Reset Password